Chuo kinatoa kozi ndefu na fupi umuwezesha kijana ajikwamue kiuchumi na kupunguza tatizo la
ajira.
Chuo kinapatikana Mkundi mwisho katika manispaa ya Morogoro.
Kipo katika mazingira tulivu na salama kwa malezi bora ya
mwanafunzi.
Chuo ni cha kutwa na bweni ambapo wanafunzi wa
bweni wanapata huduma za chakula pia.
JITA imeanzishwa tangu mwaka 2016. Ni chuo pekee kilichoanzishwa kutokana na utafiti wa muda mrefu kuhusu
ongezeko la wahitimu wa kidato cha nne baada ya juhudi za serikali kuanzisha shule za sekondari kila kata kwa
lengo la kumuwezesha kila mtanzania kupata elimu walau ya sekondari.
Kutokana na utafiti huo, iligundulika kuwa vijana wengi wanahitaji elimu ya ufundi ili kujipatia kipato kwa
maendeleo zaidi.
JITA inaamini kuwa, kwa kumuwezesha kijana kielimu hasa elimu ya ufundi, unamjengea uwezo wa kujiamini na
kujitafutia kipato na kupunguza utegemezi katika jamii.
JITA Tunasema, “MWENYE UJUZI HALALI NJAA”