KWANINI UCHAGUE CHUO CHA UFUNDI JITA?
- Mazingira mazuri na tulivu ya kujifunzia
- Darasani ni vitendo zaidi
- Elimu za ujasiriamali kwa wanafunzi
Chuo cha ufundi JITA kilianzishwa mnamo tarehe 11.4.2016 na kimesajiliwa na NACTVET kwa namba REG/NACTVET/VTC/0845 kutoa mafunzo ya ufundi kwa kozi za muda mrefu katika fani za;
Na pia chuo kinatoa mafunzo kwa kozi za muda mfupi katika fani za;
Chuo cha JITA kinapatikana katika kata ya Mkundi, manispaa ya Morogoro km 10 kutoka stendi ya Msamvu kuelekea barabara ya Dodoma.
Wanafunzi
Kozi
Waalimu
Kuwa chuo bora cha ufundi Tanzania chenye kumjenga mtu kitaaluma, kiuchumi, kimaadili na kutokomeza umasikini katika jamii.
Kuhamasisha, kuelimisha na kulea vijana katika misingi ya kimaendeleo kuhakikisha tunajenga taifa Imara.
Course Tunazotoa
800,000
Utasoma mambo yote ya salon kwa undani, kwa vitendo na pia elimu ya maisha, customer care na communication skills
800,000
Hapa utafundishwa kushona na kudizaini aina zote za nguo na pia kudarizi mashuka, vitambaa nk. Utafundishwa kwa undani na kwa vitendo zaidi.
300,000
Hapa utafundishwa kudarizi mashuka, vitambaa, nguo za aina mbalimbali. Hii ni kozi fupi ya kudarizi ambayo anasoma mtu yeyote hata kama hajui kusoma na kuandika.
300,000
Hapa utafundishwa kufuma masweta, kofia, soksi nk dizaini zote kwa mashine za kadi na za kawaida. Ni kozi fupi kwa ajili ya mtu yeyote bila kujali elimu, umri wala jinsia. Ni kozi nzuri yenye fursa kubwa mtaani kwani shule zinazohitaji masweta ni nyingi na wafumaji ni wachache. Inachukua muda wa miezi miwili tu
300,000
Hii ni kwa ajili ya mtu yeyote bila kujali elimu yake wala ufaulu.. Ni kozi inayolenga kumpa mtu ujuzi na uwezo wa kushona nguo aina mbalimbali pamoja na kudizaini mavazi. Hii inafundishwa kwa vitendo zaidi nguo za kike na za kiume.
300,000
Hapa utafundishwa kuoka keki zaidi ya aina 6 pamoja na kuzipamba. Kama keki za harusi, birthday, send off, kitchen party. Unaweza kutumia fondant, lace, wofer paper, nk
600,000
Hii ni fani ya salon inayochimba kiundani maswala yote ya salon kuanzia kusuka mitindo mbalimbali ya kiubunifu, make up aina zote, facial, manicure, pedicure, malemba, kuset, weaving, dread nk. Pia, somo la customer care wanafundishwa kwa lengo la kumuwezesha mwanafunzi aweze kuwasiliana na mteja wake kwa ufanisi mkubwa na kuwavutia wateja zaidi. Wanapata muda mwingi wa kufanya mazoezi kwa vitendo. Na hii ni kwa mtu yeyote hata kama hajui chochote anakaribishwa
400,000
Hapa kutokana na muda kuwa mfupi, mwanafunzi anafundishwa mambo muhimu tu ili aweze kuingia mtaani mapema na kuanza kujipatia pesa kupitia ujuzi wake. Utafundishwa misuko yote muhimu na yenye wateja wengi kama yeboyebo, vitunguu, knotless, croachet, dread (kurepair na kuanzisha) stitch, flat twist nk pia maswala yote ya urembo kuanzia weving, wanja, malemba, mibano, make up zote, kuset, kubond, kushonea, steaming nk.
400,000
Katika kozi hii utafundishwa kanuni na taratibu za upambaji katika matukio tofauti tofauti, Namna ya kupamba kwa mafanikio makubwa, stage designing, kupamba magari aina tofauti tofauti, kupamba kumbi mitindo ya kisasa na kwa kutumia vifaa vya kisasa. Pia utafundishwa kwa vitendo zaidi katika kumbi tofauti tofauti ndani na nje ya Morogoro.